| italiano | english | swahili | português |
   
 

 

EPISODI ILLUSTRATI
CANTI
BIBLIOGRAFIA
LA CAUSA DI BEATIFICAZIONE
DOVE SIAMO

home | mail | guestbook | links

Mtunzi: Renato Riccioni (Mtetezi wa Utakatifu wao)
Mfasiri: nd. Rikardo Maria Riccioni

gruppo bronzeoTangu mwaka 1989 uwanda uliopo katikati ya mji wa Fiuggi umepambwa na sanamu za shaba zilizowekwa mahali pa wazi, pamoja na vigae vinne vilivyobandikwa upande wa mbele wa kanisa la Imakulata; kazi hizo za msanii Angelo Canevari zinakumbusha akina dada watatu wa wilaya ya Ciociaria ambao mwaka 1741, kufuatana na wiki za uamsho zilizohubiriwa na mapadri Tommaso Struzzieri na Gaetano Giannini, walikuwa wa kwanza kuwajibika na "(…) katika nyumba yao iliyokuwa chini ya kanisa la parokia ya Mt. Stefano (…) waliamua kutawa; jambo hilo lilipojulikana katika eneo lile, wasichana wengine walikusanyika huko mchana ili kutimiza ibada zao. Halafu, juhudi zao zikiongezeka, walifungua huko aina ya shule ili kuelimisha wasichana katika misingi ya dini yetu takatifu". Ndivyo vyanzo vya wakati ule vinavyosimulia kifupi asili ya “safari yao takatifu” iliyofaidisha wasichana wa mji huo kabla haijaenea katika ujirani na hata kuvuka bahari.

targaKatika mpando, kutoka huo uwanda Trento na Trieste, unaanza “Barabara ya akina dada Faioli” inayoitwa hivyo kwa heshima ya hao Walezi-Waanzilishi watatu ambao karibu kwenye barabara hiyo tu waliishi hali yao ya kuwekwa wakfu kwa Mungu katika huduma nyenyekevu ya malezi ya msingi upande wa utu na wa dini.

Teresa (aliyezaliwa tarehe 2 Desemba 1715), Cecilia (aliyezaliwa tarehe 28 Februari 1719) na Antonia (aliyezaliwa tarehe 10 Juni 1723), walipofiwa mama yao walikuwa na umri wa miaka 12, 8 na 4, lakini hawakukubali kukata tamaa: walijikaza na, kupitia vifaa bora vya maisha ya Kikristo yaliyotekelezwa vizuri, walizaa matunda yaliyoweza kuchangamsha wananchi wenzao, kupata kibali cha Maaskofu, kuvuta wasichana wengine ambao wakaja kufungua shule sehemu nyingine pia.

Wakitegemezwa na Paroko wao mstahiki – Dekano Domenico Girolami, rafiki wa Mt. Paulo wa Msalaba – aliyewatungia Kanuni ya awali ambayo ikaja kupitishwa na Askofu Giannantonio Bacchettoni mwaka 1747, akina dada Faioli walianzisha Bweni la Anticoli, taasisi iliyofuata mfano wa kazi ya maendeleo iliyofanywa miaka ya 1700 na Watawa Walimu wa Montefiascone; ambao akina Faioli walivaa kanzu yao karibu maisha yao yote, hadi ilipokubalika Kanuni mpya iliyotungwa na Askofu Cirillo Antonini, aliyewapa kanzu ya kitawa ya Mt. Klara mwaka 1781: ndivyo lilivyoanza Shirika la Masista wa Imakulata wa Mt. Klara. Badiliko la muundo lilikamilika tarehe 4 Juni 1786 ambapo Antonini alipokea nadhiri yao ndogo ya useja mtakatifu, na hao Watawa Walimu wakawa masista kamili. Ndiyo hatima ya matukio yasiyokosa upinzani na magumu vilivyovumiliwa kishujaa kwa kimya na juhudi mpya daima.

Anayetaka kupata picha sahihi ya Bweni la Anticoli ni lazima azingatie Kanuni ya awali: "Lengo kuu la Bweni na la shule liwe kuishi kwa umakinifu na kuongea na Mungu" kwa sababu "walimu wasio na roho ya Mungu wanafaa kubomoa shule kuliko kuzijenga".

Vilevile ni lazima kuzingatia matunda ya msimamo huo, kwa kuwa utafiti wa kihistoria unaonyesha mambo ya maana sana: kati ya walelewa waliotoka mbali, tunamkuta mama wa Mt. Maria De Mattias, na kuhusu masista wawili waliotumwa wafungue shule huko Ferentino, alitoa sifa zao mmojawapo wa wale waliofaidika, Mwenye Heri Caterina Troiani.

Bila ya shaka, huo uzazi mkubwa wa kiroho ulitokana na machaguo makali: walijinyima Kifransisko mali yao yote, kwa hati rasmi mbele ya wakili, ili wamtumikie Mungu tu "ambaye, ili kumpendeza na kumtumikia kikamilifu, tukiachana na ubatili wa ulimwengu, tumetawa kwa radhi kabisa", kama alivyotamka Antonia wakati wa Mkutano wa mwaka 1781. Katika ripoti rasmi ya tarehe 22 Agosti 1779 kwa Papa Pius VI, siku chache baada ya kifo cha Teresa, Askofu Antonini mwenyewe alikariri hivi maneno ya Muungamishi asiye wa kawaida aliyeteuliwa naye kwa jumuia ya Bweni: "(…) kadiri ya dhamiri yake anatakiwa kuniambia tena ananiambia kwa heri ya kimbingu, kuwa amekuta Njiwa wengi na Bibiarusi wengi wa Yesu, waliofundishwa kuhusu njia ya Bwana kwa uangalifu wa hali ya juu, kwa usahihi makini kabisa (…) hivi kwamba kwa moyo wote wanajitahidi kumpenda, kumtumikia na kumtukuza, wakishughulikia kweli ukamilifu kwa juhudi ya hali ya juu”; akaongeza, "mimi mwenyewe, miezi michache baadaye, wakati wa ziara ya kichungaji niliyofanya katika eneo lile, nilichunguza kwa kila namna tabia zao, mienendo yao, maadili yao nikajengeka sana kwa habari nilizozipata kila mahali kulingana na matarajio yangu".

Kuhusu sifa maalumu za kila mmojawapo wa akina dada hao watatu, “waliojizoesha muda wote wa maisha yao katika maadili ya Kikristo”, maneno ya kutuangaza yanapatikana katika “Kitabu cha kumbukumbu ya akina dada marehemu” ambacho kinawatambulisha hivi: Teresa (aliyefariki tarehe 14 Julai 1779) “hasa katika upendo wa jirani kwa kumtumikia kwa huduma nyenyekevu na kwa kimya”; Cecilia (aliyefariki tarehe 13 Desemba 1789) “hasa katika sala takatifu na busara”; Antonia (aliyefariki tarehe 21 Januari 1793) “alikuwa na juhudi na bidii katika kumtumikia Mungu akitimiza maadili yote, na kupenda hasa usafi wa moyo kwa maneno na matendo vilevile”.

Shirika la Masista wa Imakulata wa Mt. Klara walilolianzisha, hatimaye likawa na hadhi ya Kipapa mwaka 1957 kwa decretum laudis ya Papa Pius XII. Shirika, likizingatia sifa ya utakatifu wao ilivyozidi kuvuma, liliomba mwaka 1987 ifunguliwe kesi ya kuwatangaza watakatifu. Hatua ya kijimbo ya kesi hiyo ilikamilika tarehe 1 Julai 1990 lakini utafiti wa kihistoria unaendelea ili kuzidi kuthibitisha maisha, maadili na sifa ya utakatifu ya hao Watumishi wa Mungu watatu.

Masalia yao, pamoja na yale ya wenzao wa kwanza, yanatunzwa katika kanisa la Imakulata huko Fiuggi, yanapotembelewa na watu wengi ambao wanasali huko na wanapenda kuacha kwa maandishi maombi na shukrani kutokana na fadhili walizojaliwa.

 

Renato Riccioni
Mtetezi wa Utakatifu wao

Mfasiri: nd. Rikardo Maria Riccioni


Kabla ya Juni 1687 – Familia ya babu Feliche kuhamia Anticoli
Anticoli, 1709 – Fransisko kumuoa Marta: historia kuanza katika familia
11 Desemba 1715 – Teresa kuzaliwa, akiwa binti wa kwanza wa Fransisko na Marta
28 Februari 1719 – Teresa kumpokea katika familia mdogo wake Sesilia
19 Juni 1721 – Teresa kupewa mapema Kipaimara na Askofu Yohane Mbatizaji Bassi
10 Juni 1723 – Antonia kuzaliwa: siku ya kwanza ya Dada Watatu kuwa pamoja
1723-1727 – Dada Watatu katika familia, shule ya kuingia vema katika jamii
Maisha ya kila siku – Pamoja na familia kutambua siku ya Bwana
Maisha ya kila siku – Mnadani, kuchagua ili kununua kwa uangalifu
Maisha ya kila siku – Familia ni shule ya uwajibikaji
Maisha ya kila siku – Kujifunza toka kwa mama ili kukua
Maisha ya kila siku – Sala mezani kufundisha shukrani
Mnamo Septemba 1727 – Kukabili pamoja na mama fumbo la uhai
17 Oktoba 1727 – Maria kuzaliwa kwa shida
17-20 Oktoba 1727 – Kihoro cha watu wawili, halafu kifo cha mtoto mchanga
21 Oktoba 1727 – Mama kuaga dunia kisha kumpokea Yesu
22 Oktoba 1727 – Mama kutoka nyumbani kwa mara ya mwisho
22 Oktoba 1727 – Mama kutoonekana tena, lakini Yesu amefufuka
15 Juni 1728 – Kuimarika na kutoa ushuhuda: Kipaimara kwa Sesilia na Antonia
Maisha ya kila siku –  Kudumisha moto ili kuleta joto na mwanga
Maisha ya kila siku – Maji ni mazuri, lakini ni lazima kuyachota
Maisha ya kila siku – Nguo zilizofuliwa kunukia sadaka
Maisha ya kila siku – Liturujia na ibada za kujichagulia, nafasi za malezi
Mnamo Mei 1734 – Kukua kati ya matatizo ya jamii
Juni 1734 – Kushiriki kanisani kwa kusikiliza wachungaji
Baada ya 20 Septemba 1736 – Padri mpya toka Anticoli: Dominiko Girolami
1737-1740 – Watu mahali pao katika mipango ya Maongozi ya Mungu
19 Januari 1740 – Padri Dominiko Girolami kuteuliwa padri mkuu wa Anticoli
29 Juni 1740 – Maji kuharibu mazao shambani: majani tu kuwa chakula Anticoli
13 Novemba 1740 – Heshima ya mwisho ya Akina Dada Faioli kwa baba yao Fransisko
Baada ya 13 Novemba 1740 – Dada Watatu kuanza kufikiria maisha yao ya baadaye?
Kabla ya Juni 1741 – Padri Girolami kutangaza wiki za uamsho
Juni 1741 – Wiki za uamsho kutikisa Anticoli
Kuanzia Juni 1741 – Ardhi tatu zenye rutuba kuitikia wito
Baada ya Juni 1741 – Uamuzi wa Dada Watatu kutawa
23 Novemba 1741 – Abati Rosa kumrithisha Teresa kwa wasia
Mwisho wa Desemba 1741 – Ukaguzi kwa ajili ya kutumia vema riziki
Baada ya 23 Desemba 1741 – Machaguo ya wasichana kama walezi
7 Septemba 1742 – Urithi kupingwa kisheria: Teresa mahakamani
1741-1747 – Kundi la sala kugeuka aina ya shule
29 Julai 1746 – Kuagana na kaka Arkanjelo pia
7 Julai 1747 – Lebo ya Askofu kwenye nyumba-shule ya Akina Dada Faioli
7-9 Julai 1747 – Jioni za siku tatu kwa sherehe za kimalezi
16 OKtoba 1747 – Askofu Bacchettoni kukagua karama ya Akina Dada Faioli
Novemba 1747 (?) – Padri Girolami kuwakabidhi Dada Watatu Roza, mtoto wa ndugu yake
Desemba 1747 – Kutengeneza na kuhamia Nyumba Mama
25 Desemba 1747 – Ufunguzi rasmi wa Bweni la Imakulata
7 Januari 1748 – Jaribio la ukomavu kwa kutengana mapema
7 Januari / 3 Mei 1748 – Teresa huko Anagni pamoja na Dominika Tardioli
26 Januari 1748 – Mtakatifu mlinzi duniani kutetea kazi ya Mungu
24 Juni 1748 – Papa Benedikto XIV kufadhili Bweni
4 Novemba 1748 – Mjane kwenda kwa wakili ili kujitoa kwa Bweni
17 Machi 1749 – Mtihani kwa Watawa Walimu
8 Novemba 1749 – Kujitoa kabisa pamoja na mali yote
1 Desemba 1749 – Askofu Bacchettoni kuhamishwa na kuendelea kusaidia toka mbali
16 Mei 1750 – Ushahidi mzuri wa Gavana
Agosti 1752 – Jumuia fukara na pweke kudumu katika matatizo
Baada ya 22 Januari 1753 – Mkurugenzi kurudi kisha kutambulika hana makosa
2 Julai 1753 – Ziara kali ya kichungaji
Maisha ya kila siku – Ulimwengu kusumbua kishenzi kwa kelele, dhihaka na matusi
5 Septemba 1753 – Mkurugenzi kurudishiwa nyumbu aliyekamatwa
27 Aprili 1757 – Ufukara na hatari: kati ya mahangaiko na Maongozi ya Mungu
Juni 1759 – Anjelika Bertoni kurudi na baada ya miezi michache kufanywa mkuu wa jumuia
5 Juni 1760 – Mlelewa Kolombina kurukia ahera
7 Februari 1763 – Askofu Monti kuwalipia shela za Watawa Walimu kama utambuzi usio rasmi
24 Oktoba 1773 – Patakatifu pia panaweza pakaanguka, lakini heshima kwa Maria siyo
1 Agosti 1774 – Ziara ya Askofu Filipponi Tenderini na sharti lake
14 Machi 1775 – Lwiza Borsetti, mtoto yatima wa miaka sita, kuingia
6 Machi 1779 – Anjelika Bertoni kujiuzulu ili kutoka; Antonia Faioli kuchaguliwa mkuu wa jumuia
6 Machi 1779 – Baada ya Anjelika Bertoni kujiuzulu, jumuia kumchagua Antonia
23 Aprili 1779 – Katika ziara ya kwanza ya kichungaji, Askofu Sirili Antonini kuridhika sana
Kabla ya 14 Julai 1779 – Teresa kumaliza huduma yake duniani
23 Agosti 1781 – Mageuzi ya Kifransisko: Watawa Walimu kuwa Masista wa Mt. Klara
8 Novemba 1781 – Antonia kuongoza jumuia ikubali kanuni mpya
Baada ya 12 Julai 1785 – Mtakaji bora kujiunga: pamoja na dada Manaccioni kuelekea kesho
6 Agosti 1785 – Padri shujaa Girolami pia kumaliza maisha yake yenye mateso
29 Januari 1789 – Askofu Antonini pia kuitwa kwenye tuzo la milele
4 Juni 1786 – Kwa nadhiri ya kitawa, uwajibikaji katika kushika mashauri matatu ya Kiinjili
13 Desemba 1789 – Sesilia kudumisha moja kwa moja sala yake
21 Januari 1793 – Dada Watatu kuungana tena: ndio mwisho wa kipindi cha asili
Milenia ya tatu – Njia ya Dada Watatu baada ya maisha yao

 

 

© 2007 - Congregazione delle Suore dell'Immacolata di Santa Chiara
- DIADAIN consupertrafra -